top of page
Writer's pictureBranice Nafula

'Huu Mwaka Mtaniita Bosi" Miongoni mwa Nyimbo Zingine Kali Kuhusu mwaka 2024



[Image Source: Instagram]

Writer: Elizabeth Betha

Kuanza na kuingia mwaka mpya ni kitu cha furaha na kilichojaa matumaini mapya, ndoto mpya, mipango na mikakati na kwa wengine malengo mapya kabisa.


Kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania, wasanii wameonesha ubunifu wa kuja na midundo yao inayozungumzia mambo ya mwaka mpya, na humo ndani wametumia akili nyingi kuhakikisha jumbe zao zinagusa watu kwa ukubwa sana, na nyimbo kuchezeka na kuimbwa kwa urahisi. Kiufupi ubunifu na maandalizi mazuri kwenye uandishi na utayarishaji wa kazi zao unasadifu matokeo waliyoyapata kupitia nyimbo walizozitoa zinazozungumzia mambo ya mwaka mpya.


Harmonize alitupa ‘anthem’ yake ya ‘Mwaka Wangu’ miaka miwili iliyopita lengo ilikuwa kuwapa moyo maashabiki na watu kwa ujumla, kupambania ndoto zao kwenye mwaka ili wafikie malengo yao, ukiachana na kuimbika ni wimbo uliobeba ujumbe mzuri na kiukweli ulifika kitaani.


Dayoo alitupa ‘Huu Mwaka’ ambayo ni wimbo uliopata mafanikio makubwa sana kwa minajili ya ujumbe wake uliochangamka, unachezeka, unaimbika, ulifanyiwa challenges za kutosha kwenye mitandao kama TikTok na ukapata ‘remix’ kali akimshirikisha Rayvanny ambayo nayo ilifanikiwa sana. Dayoo aliimba;-

“Huu mwaka eeh, ni mwaka wa kuforce

Yaani mtake msitake, huu mwaka mtaniita boss”.



Hivi karibuni kwa maana siku ama wiki za karibuni wasanii kadhaa wameachia nyimbo zao zinazozungumzia mwaka mpya, na Dayoo kupitia kurasa yake ya mtandao wa kijamii aliandika kuashiria anasikia faraja kuona wasanii wenzake wamekuwa ‘inspired’ na yeye na kuachia nyimbo zenye maudhui kuhusu mwaka.


Ibraah the King of New School, amechia wimbo wake wiki mbili zilizopita unaojulikana kama ‘Nafunga Mwaka’ ni ‘anthem’ ya kuiambia mitaa na wananchi wake kufurahia mwaka unaoisha na kushukuru kwa yote yaliyotokea mwaka huu, ni goma la kufungia mwaka na kujiandaa na mwaka unaokuja, kama ambavyo King of New School anavyoimba:

“Oya nafunga mwaka ooh, tukutane mwakani!”


Aslam TZ msanii chipukizi wa BongoFlava nae ameachia wimbo wake unaoitwa ‘Tukutane Mwakani’, ni ujumbe mzuri wa kufariji na kujipanga na mwaka unaokuja, Aslam hakuishia kuimba mwenyewe, ameachia ‘remix’ ya wimbo huo akiwa amewashirikisha Mabantu na Masauti kutoka nchini Kenya, ambao wote kwa nafasi zao wameongeza ladha ya tofauti na kuuongezea ubora, Aslam ameimba;-


“Mwakani tuombe Mungu sana, maana hakuna kinachoshindikana

Ohh mwakani si ndo matajiri wa mwakani, ooh mwakani si ndo maboss wa mwakani”

Kati ya ngoma hizo mpya na zilizotoka mapema zaidi ipi unaikubali zaidi, share hapo kwenye sehemu ya comment, halafu kama vipi tukutane mwakani!

0 views0 comments

Comments


bottom of page